Habari
rafiki,
Ni
matumaini yetu kuwa umeinza siku yako vyema kabisa ukiwa na afya njema, tuna
kila sababu ya kukupongeza kwa hilo kwani si kila aliyeianza siku ya leo
anaafya njema kwani afya njema inatengenezwa na haiji kwa bahati.
Leo ni ile
siku yetu maalumu ya kupeana maarifa kuhusu afya ya uzazi kama ilivyodesturi
yetu. Katika somo letu la leo tutajifunza kuhusu tatizo la kuwahi kutoa mbegu za
uzazi (manii) au kufika kileleni kwa wanaume punde tu mwanaume anaponza
kushiriki tendo la ndoa.
Kama
tunavyofahamu kuwa hili ni tatizo na limekuwa likiathiri idadi kubwa ya wanaume
kwa sasa na limekuwa na tafsiri tofauti katika jamii yetu na hata kupelekea baadhi
ya ndoa kuvunjika.
Tuungane kwa pamoja tukajifunze somo
hili……
Kuwahi
kutoa manii mapema baada tu ya kunza tendo la ndoa kwa kitaalamu tunaita
(Premature ejaculation) ni kitendo cha kutojizuia kutoa manii aidha kabla au
baada ya sekunde chache kuanza kwa tendo la ndoa.
Tatizo hili
husababisha kutokuridhika au kutofurahia tendo la ndoa kwa wanandoa wote wawili
(mwanaume na mwanamke). Na hali hii husababisha uoga kwa wanandoa na kupelekea
kuongezeka kwa tatizo maradufu.
Ni sababu gani hasa husababisha
kuwahi kufika kileleni (premature ejaculation)?
Mpaka sasa
hakuna sababu za moja kwa moja zinazosababisha kuwahi kufika kileleni kwa
mwanaume (orgasm).
Wakati
mwengine tatizo hili hutokana na hali ya mazingira wakati wa tendo la ndoa,
uoga uliopitiliza (anxiety), msongo wa mawazo (depression).
Vile vile
husababishwa na tatizo la vichochezi vya mwili vinavyohusika na uzazi (hormonal
problems), majeraha hasa sehemu za kichwa (brain injury) na hata matokeo yasiyotarajiwa
kwa baadhi ya dawa (drug side effects).
Ni zipi dalili za kuwahi
kufika kileleni (orgasm) kwa wanaume?
Dalili
kubwa ni kushindwa kujizuia kutoa manii kabla au muda mfupi baada ya kuanza
tendo la ndoa, kutoka kwa manii pasipo mwanaume kutarajia.
Tiba yake ni ipi?
Kwa baadhi
ya wanaume tatizo hili hupotea baada ya muda mrefu, kwa wanaume wanaotumia
kilevi aina ya pombe au kuvuta sigara wanatakiwa kuacha mara moja na inaweza
kuimarisha utoaji manii mzuri.
Vile vile
zipo dawa za kuondoa tatizo hilo mara moja na kuimarisha mfumo mzuri wa mwanaume
wa utoaji manii wakati wa tendo la ndoa na kupelekea kumridhisha mwenza wake na
kufurahia tendo la ndoa.
Hapo
tumefikia mwisho rafiki katika somo letu siku ya leo, tukutane tena kwenye
mwendelezo wa masoma ya afya ya uzazi wiki ijayo siku kama ya leo. Pia
tutakutana tena kesho kwenye kipindi cha makala ya AFYA BORA.
Tunakutakia
kila la kheri,
“Afya
bora ndio msingi wa mafanikio yako”
Kwa maoni, ushauri, TIBA NA DAWA, Piga simu namba: 0652028582 au 0652394698 au 0654502550.
Whatsap group: AFYA NI YANGU,
Facebook Page: Afya Ni Yangu.
#TRIPLE MINDED.
Jaza form hii kupokea makala za Afya Ni Yangu.
No comments:
Post a Comment