Habari yako
rafiki,
Leo ni siku
nyingine tena tunakutana, leo ni jumamosi tulivu kabisa. Ni matumaini yetu kuwa
unaendelea vizuri na unaendelea kuwa makini sana na afya yako kwa ujumla, na tunauhakika
kuwa haupo tayari kuruhusu mtu/kitu chochote kicheze na afya yako. Ndiyo, afya
yako ni ya thamani sana.
Leo
tunaungana moja kwa moja kwenye kipindi chetu cha leo cha huduma ya kwanza
(First Aid).
Huduma ya
kwanza sio neno jipya kabisa katika masikio au macho yetu, tumeshalisikia sana
na tumeshalizoea. Pia kuna baadhi yetu wamesha wahi kutoa huduma ya kwanza kwa
mtu ambaye anahitaji kupatiwa huduma ya kwanza.
Ni vizuri
sana kuwa na ujuzi wa kutoa huduma ya kwanza kwa kila mmoja wetu pale tu inapohitajika,
leo tutachambua kwa kina kuhusu huduma ya kwanza.
Kwani huduma ya kwanzinakuaje/inafanyikaje?
Huduma ya
kwanza ni msaada wa haraka sana unaotolewa kwa mtu yoyote ambaye yupo katika
hali ya kuhatarisha au kupoteza maisha yake.
Huduma ya
kwanza inaweza kutolewa kwenye dharula kama zifuatazo; mtu alikunywa sumu,
aliyeng’watwa na nyoka (Nge, Nyuki, au mdudu yoyote mwenye sumu kali), aliye
ungua, aliyepatwa na jeraha lenye kutoa damu nyingi, aliyepatwa na kifafa,
aliyepoteza fahamu ghafla, aliyezimia, aliye paliwa, aliye zama maji na dharula
nyengine nyingi.
Ni kitu gani napaswa
kuzingatia napotoa huduma ya kwanza?
Kwanza
kabisa ni muhimu sana kujua mambo ya msingi kabla ya kutoa huduma ya kwanza.
1. Hakikisha unaujuzi wa kutoa huduma
ya kwanza kulingana na tukio husika, usijaribu kutoa huduma ya kwanza endapo
huna ujuzi huo kwani yaweza kuongea hatari zaidi kwa mgonjwa na hata kwako pia.
2. Hakikisha unapotoa huduma ya kwanza
wewe unakuwa salama, kwani unaweza kutoa huduma ya kwanza ikapelekea
kuhatarisha maisha yako pia.
3. Hakikisha unakuwa na vifaa
vinavyotumika kutolea aina husika ya huduma ya kwanza (kama inahitajiaka).
4. Inapotokea dharula inayohitaji
huduma ya kwanza, fanya yafuatayo;
a) Yakupasa uchunguze au uulize nini
kimetokea. Itakusaidia kujua uanzie wapi kulingana na dharula husika.
b) Je, mazingira yanakuruhusu kutoa
huduma ya kwanza?
c) Mgonjwa yupo eneo salama ambalo linakuwezesha
kutoa huduma ya kwanza pale alipo pasipo mgonjwa hudhurika zaidi?
Ikiwa kuna
dharula imetokea na imeathiri zaidi ya mmoja yakupasa kuweka kipaumbele
(Priorities) kulinana na hali zao.
Nitawezaje kuweka
kipaumbele(priorities) endapo kuna watu wengi walipatwa na dharula na kila
aliyedhurika anahitaji msaada?
Tukutane
tena kwenye kipindi kijacho rafiki, tutaendelea na somo letu la huduma ya
kwanza.
Tukutakie
kila la kheri, tukutane tena kesho kwenye vipindi vya makala zinazoendea.
Tunakaribisha
maswali kuhusiana na somo letu la leo kuanzia sasa.
Karibu.
Kwa maoni, ushauri, TIBA NA DAWA, Piga simu namba: 0652028582 au 0654394698 au 0654502550.
Whatsap group: AFYA YA UZAZI NA MTOTO,
Facebook Page: AFYA YA UZAZI NA MTOTO.
#TRIPLE MINDED.
Jaza form hii kupokea makala za Afya Ni Yangu.