1. SWALI
LA LEO
2. AFYA
BORA
3. AFYA
YA UZAZI
4. AFYA
YA MTOTO
5. ONGEA
NA MSHAURI
6. MASWALI
NA MAJIBU
7. CHANGAMOTO
YA SIKU
8. KLIINIKI
YA MAMA NA MTOTO
9. HUDUMA
YA KWANZA (FIRST AID)
10.
MEDICAL & SURGICAL CONDITIONS
SWALI LA LEO;
Ni
kipindi kitakacho fanyika siku ya jumatano, swali ambalo litawekwa mezani na
wataalamu wa afya (uongozi wa mtandao wa AFYA NI YANGU). Swali ambalo
litakuhitaji ufikiri wa kina ili kupata jibu sahihi, majibu yote yatakayojibiwa na wanachama wa kundi hili yatafanyiwa
kazi na uongozi.
AFYA BORA;
Ni
makala itakayo rushwa siku ya jumanne, hii ni aina ya makala itakayo kuongezea
maarifa kiundani zaidi kuhusu umuhimu wa kuwa na afya bora, namna gani unaweza
kuwa na afya bora wakati wote na kuimarisha afya yako kwa ujumla.
AFYA YA UZAZI;
Ni
aina ya makala itakayorushwa siku ya jumatatu, hapa utapata kujifunza magonjwa
ya aina yote ya uzazi kwa mwanamke na mwanaume
pamoja na tiba/dawa sahihi.
AFYA YA MTOTO;
Ni
makala itayorushwa siku ya alhamisi, itakayozungumzia hasa afya pamoja na
magojwa ya watoto kuanzia akiwa kijusi (fetus)
– kichanga (Neonate/Infancy) – hadi
miaka kumi na moja (Children). Ni
siku muhimu sana kwani utapata kuyafahamu mengi kuhusu watoto, kwani watoto ni
sehemu ya furaha katika maisha ndoa na familia kwa ujumla.
ONGEA NA MSHAURI;
Huu
ni wakati wa mwanachama wa mtandao huu kupata fursa ya kuongea na mshauri moja
kwa moja kwa kupiga simu, kwa siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tano
asubuhi hadi saa nne usiku.
Ushauri
utakaotolewa ni wa magonjwa ya aina yoyote ya binadamu na kupatiwa ushauri na ufumbuzi
wa tatizo husika.
N.B.
Hairuhusiwi kutuma ujumbe (sms), hivyo
ujumbe utakaotumwa hautafanyiwa kazi na uongozi husika.
MASWALI NA MAJIBU;
Hapa
mwanachama atapata fursa ya kuuliza maswali husiana na magonjwa ya aina yote ya
binadamu, kipindi hiki ni kwa siku ya Ijumaa tu. Hapa mwanachama atapata fursa
ya kuwasilisha swali lake kwa njia ya ujumbe wa wa maandishi (whatsap group, inbox) au kwa kupitia e mail
yetu (afyaniyangu@gmail.com)..
CHANGAMOTO YA SIKU;
Hapa
utapokea makala itakayo elezea suluhisho la miongoni mwa changamoto
zinazowasumbuwa watu wengi kuhusu afya zao hasa wale wanaotufikia moja
kwa moja na wale wanaotupigia simu pia. Makala hii itaandaliwa siku ya ijumaa
pekee. Hivyo tutakushirikisha na tutajifunza kwa pamoja.
KLINIKI YA MAMA NA MTOTO;
Hii
ni huduma maalamu itakayotolewa kwa mfumo wa makala kuelezea huduma anazopaswa kupewa mama mjamzito
kuanzia anapoingia kliniki hadi anapotoka, vile vile huduma anazopewa mtoto
pale anapoingia kliniki hadi kutoka.
Hapa
utajifunza mambo mbalimbali kama vile;
- · Maana ya kila huduma anayopewa mama mjamzito anapokuwa kliniki.· Maana ya kila hatua anayoifuata mama mjamzito anapokuwa kliniki.· Umuhimu wa dawa/chanjo anazopewa mama akiwa kliniki.· Elimu anayopewa maam akiwa kliniki.· Vipimo anavyotakiwa kufanyiwa anapokuwa kliniki na mengine mengi.
Huduma
hii ya KLINIKI YA MAMA NA MTOTO
itatolewa kwa njia ya mtandao wa facebook page na whatsap ‘Afya Ni Yangu’ kila
jumapili kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nane mchana.
Itafanyikaje
kupitia mtandao?
Hapa
tutakuwa kliniki na mama, mwanamke na hata wananaume wenye kujali na kuthamini
afya za wake zao au wanawake pamoja na mtoto wao mtarajiwa, ili kupata somo
hili inakubidi mwanachama awe anatumia kifaa chochote kinachomuwezesha kuwa na
mtandao wa kijamii kama vile smartphone au tablet ambapo anatakiwa kuwa online
siku hiyo na wakati wa somo husika.
Itakuwaje
kama sipo online kwa muda huo?
Bado
hujapoteza kitu moja kwa moja kwani endapo utafungua mtandao wako utakutana na
somo lililokuwa likiendelea siku hiyo, ispokuwa utakosa fursa ya kuuliza swali
kuhusiana na somo au kile kinachohusiana na Kliniki ya mama na mtoto badala
yake sasa utaweza kuuliza swali hilo kwenye kipindi kijacho.
Je,
huduma hiyo ni kwa ajili ya wanawake wajawazito na wenye watoto wadogo pekee?
Hapana,
huduma hii ni muhimu sana kwa kila mtu yaani mwanaume na mwanamke kwani ni
vyema kwa wakina baba kuelewa ni huduma gani ambazo wenzi wao hupewa pindi
wanapokuwa kwenye chumba cha uchunguzi na huduma zote wanazopata wanapokuwa
kliniki kwa ujumla.
HUDUMA YA KWANZA
(FIRST AID)
Hiki
ni kipindi ambacho utaweza kujifunza ni kwa namna gani unaweza kutoa huduma ya
kwanza kwa mtu yoyote pale tu anapopatwa na tatizo la ghafla la kiafya
linalohitaji huduma ya kwanza kabla ya kumfikisha kituo cha afya.
Hili
somo ni muhimu sana kwani utakuwa unauwezo wa kuokoa maisha ya mtu endapo
tatizo litatokea ghafla eneo lolote ulilopo kama vile nyumbani, shuleni,
ofisini, mgahawani, shambani n.k
Maarifa
haya utayapata siku ya jumamosi jioni, hivyo utapaswa kuwa makini na somo hili.
MEDICAL & SURGICAL
CONDITIONS
Hapa
sasa ni ule wakati wakujifunza magonjwa ya kitabibu (kisukari, nimonia, kifua
kikuu, mafua, UTI, malaria n.k) na magonjwa ya upasuaji (Kidole tumbo, kuziba
kwa utumbo wa chakula, uvimbe n.k
Utapokea
maarifa kwa undani zaidi kuhusu magonjwa haya, ambapo itakusaidia kugundua
ugonjwa husika, dalili, vipimo vinavyohusika kugundua ugonjwa, tiba yake, namna
ya kuepukana na ugonjwa husika.
MUHIMU:
Huu ni
utaratibu mpya kabisa wa mfululizo wa masomo ya afya, kwa hakika
tutakushirikisha maarifa hayo muhimu sana katika maisha yako ya kila siku na
baada ya muda utakuwa na uelewa mpana kuhusu afya na hautakuwa hapo ulipo sasa
kifikra. Huu mfumo mpya wa makala za afya umeandaliwa baada ya kufanyia kazi changamoto
nyingi tulizokuwa tukipokea, hivyo tunaimani kuwa changamoto ni nyingi ila
tutahakikisha tunazifanyia kazi kadri ya uwezo wetu.
Shabaha
yetu kubwa ni kuhakikisha unakuwa na AFYA BORA YENYE UHAKIKA siku zote na
wakati wote.
TRIPLE MINDED.