Habari
rafiki,
Tunakubaliana
kwa pamoja kuwa watoto ni sehemu ya furaha katika maisha ya ndoa, na hilo tunalisadiki
kwa pamoja.
Linapokuja
suala la maradhi hasa kwa watoto katika familia hupoteza furaha yote katika familia.
Leo
tutakushirikisha kuhusu homa hasa kwa watoto. Homa sio ugonjwa,
homa ni dalili ya ugonjwa.
Kumekuwa na
baadhi ya wazazi wakiona watoto wao joto la mwili limepanda hutumia dawa za
kushusha joto kama vile paracetamol (Panadol), si hatua mbaya ya kuchukua
ispokuwa tatizo ni pale joto la mwili linapopanda mara kwa mara kwa zaidi ya
siku tatu mfululizo bila kuchukua hatua ya kumpeleka mtoto kituo chochote cha
afya kilichopo karibu.
Tuangalie nini maana ya jotomwili (body
temperature).
Jotomwili ni kipimo cha uwezo wa mwili kutengeneza joto,
ambapo mwili hutengeneza joto kulingana na msawazo unaotakikana hata kama joto
la nje ya mwili yaani mazingira yanayotuzunguka yatabadilika.
Inakuaje ya mwili unachemka?
Joto la
mwili linapopanda kuliko kawaida ni kwamba mishipa ya damu (blood vessels)
katika ngozi hutanuka na kubeba joto jingi kwenye ngozi ya mwili na kuanza
kutokwa jasho kupita kiasi. Na tunaposema homa tunamaanisha kupanda kwa
jotomwili (fever).
Ipi njia sahihi ya kutambua jotomwili
limepanda?
Kuna njia ya
asili ambayo tumeshaizoea kuitumia kugundua jotomwili limepanda au la, kwa
kutumia sehemu ya juu ya kijanja cha mkono (dorsum) na kugusicha kwenye mwili
wa mgonjwa. Ni njia nzuri ya awali katika kugundua jotomwili ispokuwa inakuwa
ngumu kugundua joto la mwili limepanda kwa kiasi gani.
Njia iliyo
ya uhakika ni kutumia kifaa kinachoitwa kipima joto (clinical thermometer),
hiki ni kifaa kinachotumiwa hasa na wataalamu wa afya kwenye vituo vya afya.
Kifaa hiki ni muhimu kwa kila familia kuwa nacho kwani ni rahisi kukitumia na
kukielewa.
Utajuaje jotomwili limepanda kwa kutumia
kifaa hicho (clinical thermometer)?
Kuna aina
kama mbili za kipimajoto, ya kwanza ni mercury
thermometer nay a pili ni digital
thermometer. Kwa matumizi ya nyumbani ni vyema kutumia digital thermometer
kwa urahisi wa kupata matokeo ya jotomwili.
Kiwango cha jotomwili.
Jotomwili
la kwaida ni nyuzi joto 36.5 hadi 37.5, ikitokea kipima joto kikaonesha ni
zaidi ya nyuzi joto 37.5 ni dalili ya kupanda kwa jotomwili, hivyo yakupasa
kumpeleka mtoto kwenye kituo chochote cha afya kilichopo karibu.
Muhimu;
Kupanda kwa
jotomwili kwa watoto ni dalili ya hatari ukilinganisha na watu wazima, endapo
hatua stahiki hazitachukuliwa hupelekea mtoto kupata degedege (convulsion), hivyo basi yakupasa
kumpeleka kwenye kituo chochote cha afya kilichopo karibu yako.
Tukutane
tena kwenye kipindi kijacho cha makala zinazohusu AFYA YA MTOTO siku kama ya leo, vilevile tutakutana kesho kwenye
kipindi cha makala zinazoendelea.
Tunakutakia
kila la kheri
Kwa maoni, ushauri, TIBA NA DAWA, Piga simu namba: 0652028582 au 0652394698 au 0654502550.
Whatsap group: Afya Ni Yangu,
Facebook Page: Afya Ni Yangu.
#TRIPLE MINDED.
No comments:
Post a Comment