AMUA KUSIMAMIA AFYA YAKO MUDA WOTE.




Habari rafiki,
Karibu kwa mara nyingine kwenye mtandao wa Afya ni yangu,
Kama ilivyozoeleka siku zote sisi kama wanafamilia tunashirikishana yale yaliyomuhimu sana katika sehemu ya maisha yetu ambapo bila sehemu hii ya hatuwezi kuyafurahia maisha kamwe. Sehemu yenyewe si nyingine bali ni AFYA. 

Rafiki chukua hatua mapema ya kusimamia afya yako kuanzia sasa yaani kama umefanikiwa kusoma makala hii yakupasa uanze kutafakari kwa kina kuhusu afya yako sasa, kwa maana ya kwamba hakuna mtu ambaye atakaye kusimamia katika hili ispokuwa wewe binafsi.

Kama tunavyoelewa kuwa asilimia kubwa ya maradhi yanayowakabili watu wengi yanatokana na wao, kwa mfano unapoenda hospitali ukiwa unahisi unadalili zote za malaria na ikathibitishwa na mtu wa maabara kuwa unamalaria jua ya kwamba maralia hiyo haijaingia mwilini siku hiyo yaani haujang’atwa na mbu siku hiyo hiyo na kuuguugua malaria siku hiyo.Kwa maana ya kwamba kuna kitu ulikosea hapo nyuma kuhakikisha unaepuka kuwa na maradhi ya maralia aidha ulikua hutumii chandarua wakati wa kulala, nyumba yako imezungukwa na nyasi ndefu zinazochangia mazalia ya mbu au mazingila unayoishi yamezungungwa na vidimbwi vya maji yaliyotuama ambapo mazalia ya mbu huongeza kwa wingi.


Rafiki afya ni kitu muhimu sana katika maisha yako, bila afya hakuna maisha. Kuna msemo mmoja wa Kiswahili unaosema “thamani ya afya aijuae mgonjwa”. Lakini sisi wanafamilia wa mtandao wa Afya ni yangu tunasema thamani ya afya aijuae ni mimi na wewe.


Kila inapoitwa leo, kila inapoingia asubuhi au kabla ya kuianza siku yako chukua dakika kadhaa kutafakari kuhusu afya yako ndio uanze kufanya shughuri nyingine za kiuchumi, kijamii, kisiasi na kitamaduni. Na kila unachopanga kufanya hakikisha hakiathiri afya yako.


Unatakiwa uishi kama mtu anaemiliki gari, yaani huwezi kuanza kuwasha gari kama hujalikagua gari lako kama lina mafuta ya kutosha, rejecter kama inamaji ya kutosha, mataili kama yanaupepo wa kutosha na hata kuhakikisha kama bima zote pamoja na leseni zipo sawa sawa. Baada ya hapo ndipo utakuwa salama na huru utakapokuwa barabarani.
Hivyo ndivyo ilivyo hata kwenye upande wa afya yako, kuwa makini muda wate kuhakikisha afya yako iko vyema.


 Tunakutakia kila la kheri.


Kwa maoni, ushauri, TIBA na DAWA wasiliana nasi kupitia simu namba 0654502550, 0652028582 au 0654394698.

Whatsap group: AFYA NI YANGU,
Facebook Page: Afya Ni Yangu.

 TRIPLE MINDED.

Jaza form hii kupokea makala za Afya Ni Yangu.

* indicates required
Email Format

AFYA YA UZAZI (1); Kuwahi kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa kwa wanaume (Premature ejaculation).


Habari rafiki,
Ni matumaini yetu kuwa umeinza siku yako vyema kabisa ukiwa na afya njema, tuna kila sababu ya kukupongeza kwa hilo kwani si kila aliyeianza siku ya leo anaafya njema kwani afya njema inatengenezwa na haiji kwa bahati.

Leo ni ile siku yetu maalumu ya kupeana maarifa kuhusu afya ya uzazi kama ilivyodesturi yetu. Katika somo letu la leo tutajifunza kuhusu tatizo la kuwahi kutoa mbegu za uzazi (manii) au kufika kileleni kwa wanaume punde tu mwanaume anaponza kushiriki tendo la ndoa.

Kama tunavyofahamu kuwa hili ni tatizo na limekuwa likiathiri idadi kubwa ya wanaume kwa sasa na limekuwa na tafsiri tofauti katika jamii yetu na hata kupelekea baadhi ya ndoa kuvunjika.

Tuungane kwa pamoja tukajifunze somo hili……

Kuwahi kutoa manii mapema baada tu ya kunza tendo la ndoa kwa kitaalamu tunaita (Premature ejaculation) ni kitendo cha kutojizuia kutoa manii aidha kabla au baada ya sekunde chache kuanza kwa tendo la ndoa.

Tatizo hili husababisha kutokuridhika au kutofurahia tendo la ndoa kwa wanandoa wote wawili (mwanaume na mwanamke). Na hali hii husababisha uoga kwa wanandoa na kupelekea kuongezeka kwa tatizo maradufu.

Ni sababu gani hasa husababisha kuwahi kufika kileleni (premature ejaculation)?

Mpaka sasa hakuna sababu za moja kwa moja zinazosababisha kuwahi kufika kileleni kwa mwanaume (orgasm).

Wakati mwengine tatizo hili hutokana na hali ya mazingira wakati wa tendo la ndoa, uoga uliopitiliza (anxiety), msongo wa mawazo (depression).

Vile vile husababishwa na tatizo la vichochezi vya mwili vinavyohusika na uzazi (hormonal problems), majeraha hasa sehemu za kichwa (brain injury) na hata matokeo yasiyotarajiwa kwa baadhi ya dawa (drug side effects).

Ni zipi dalili za kuwahi kufika kileleni (orgasm) kwa wanaume?

Dalili kubwa ni kushindwa kujizuia kutoa manii kabla au muda mfupi baada ya kuanza tendo la ndoa, kutoka kwa manii pasipo mwanaume kutarajia.

Tiba yake ni ipi?

Kwa baadhi ya wanaume tatizo hili hupotea baada ya muda mrefu, kwa wanaume wanaotumia kilevi aina ya pombe au kuvuta sigara wanatakiwa kuacha mara moja na inaweza kuimarisha utoaji manii mzuri.

Vile vile zipo dawa za kuondoa tatizo hilo mara moja na kuimarisha mfumo mzuri wa mwanaume wa utoaji manii wakati wa tendo la ndoa na kupelekea kumridhisha mwenza wake na kufurahia tendo la ndoa.

Hapo tumefikia mwisho rafiki katika somo letu siku ya leo, tukutane tena kwenye mwendelezo wa masoma ya afya ya uzazi wiki ijayo siku kama ya leo. Pia tutakutana tena kesho kwenye kipindi cha makala ya AFYA BORA.

Tunakutakia kila la kheri,

“Afya bora ndio msingi wa mafanikio yako”

Kwa maoni, ushauri, TIBA NA DAWA, Piga simu namba: 0652028582 au 0652394698 au 0654502550.
Whatsap group: AFYA NI YANGU,
Facebook Page: Afya Ni Yangu.

#TRIPLE MINDED.

 Jaza form hii kupokea makala za Afya Ni Yangu.

* indicates required
Email Format

HUDUMA YA KWANZA (FIRST AID): Huduma ya kwanza ni nini?



Habari yako rafiki,

Leo ni siku nyingine tena tunakutana, leo ni jumamosi tulivu kabisa. Ni matumaini yetu kuwa unaendelea vizuri na unaendelea kuwa makini sana na afya yako kwa ujumla, na tunauhakika kuwa haupo tayari kuruhusu mtu/kitu chochote kicheze na afya yako. Ndiyo, afya yako ni ya thamani sana.

Leo tunaungana moja kwa moja kwenye kipindi chetu cha leo cha huduma ya kwanza (First Aid).

Huduma ya kwanza sio neno jipya kabisa katika masikio au macho yetu, tumeshalisikia sana na tumeshalizoea. Pia kuna baadhi yetu wamesha wahi kutoa huduma ya kwanza kwa mtu ambaye anahitaji kupatiwa huduma ya kwanza.
Ni vizuri sana kuwa na ujuzi wa kutoa huduma ya kwanza kwa kila mmoja wetu pale tu inapohitajika, leo tutachambua kwa kina kuhusu huduma ya kwanza.

Kwani huduma ya kwanzinakuaje/inafanyikaje?

Huduma ya kwanza ni msaada wa haraka sana unaotolewa kwa mtu yoyote ambaye yupo katika hali ya kuhatarisha au kupoteza maisha yake.

Huduma ya kwanza inaweza kutolewa kwenye dharula kama zifuatazo; mtu alikunywa sumu, aliyeng’watwa na nyoka (Nge, Nyuki, au mdudu yoyote mwenye sumu kali), aliye ungua, aliyepatwa na jeraha lenye kutoa damu nyingi, aliyepatwa na kifafa, aliyepoteza fahamu ghafla, aliyezimia, aliye paliwa, aliye zama maji na dharula nyengine nyingi.

Ni kitu gani napaswa kuzingatia napotoa huduma ya kwanza?

Kwanza kabisa ni muhimu sana kujua mambo ya msingi kabla ya kutoa huduma ya kwanza.

1.   Hakikisha unaujuzi wa kutoa huduma ya kwanza kulingana na tukio husika, usijaribu kutoa huduma ya kwanza endapo huna ujuzi huo kwani yaweza kuongea hatari zaidi kwa mgonjwa na hata kwako pia.

2.   Hakikisha unapotoa huduma ya kwanza wewe unakuwa salama, kwani unaweza kutoa huduma ya kwanza ikapelekea kuhatarisha maisha yako pia.

3.   Hakikisha unakuwa na vifaa vinavyotumika kutolea aina husika ya huduma ya kwanza (kama inahitajiaka).

4.   Inapotokea dharula inayohitaji huduma ya kwanza, fanya yafuatayo;

a)   Yakupasa uchunguze au uulize nini kimetokea. Itakusaidia kujua uanzie wapi kulingana na dharula husika.
b)   Je, mazingira yanakuruhusu kutoa huduma ya kwanza?
c)   Mgonjwa yupo eneo salama ambalo linakuwezesha kutoa huduma ya kwanza pale alipo pasipo mgonjwa hudhurika zaidi?

Ikiwa kuna dharula imetokea na imeathiri zaidi ya mmoja yakupasa kuweka kipaumbele (Priorities) kulinana na hali zao.

Nitawezaje kuweka kipaumbele(priorities) endapo kuna watu wengi walipatwa na dharula na kila aliyedhurika anahitaji msaada?

Tukutane tena kwenye kipindi kijacho rafiki, tutaendelea na somo letu la huduma ya kwanza.
Tukutakie kila la kheri, tukutane tena kesho kwenye vipindi vya makala zinazoendea.

 Tunakaribisha maswali kuhusiana na somo letu la leo kuanzia sasa.
Karibu.

Kwa maoni, ushauri, TIBA NA DAWA, Piga simu namba: 0652028582 au 0654394698 au 0654502550.

Whatsap group: AFYA YA UZAZI NA MTOTO,
Facebook Page: AFYA YA UZAZI NA MTOTO.

#TRIPLE MINDED.


Jaza form hii kupokea makala za Afya Ni Yangu.

* indicates required

AFYA YA MTOTO (1); Homa kwa watoto


 

Habari rafiki,

Tunakubaliana kwa pamoja kuwa watoto ni sehemu ya furaha katika maisha ya ndoa, na hilo tunalisadiki kwa pamoja.

Linapokuja suala la maradhi hasa kwa watoto katika familia hupoteza furaha yote katika familia.

Leo tutakushirikisha kuhusu homa hasa kwa watoto. Homa sio ugonjwa, homa ni dalili ya ugonjwa.

Kumekuwa na baadhi ya wazazi wakiona watoto wao joto la mwili limepanda hutumia dawa za kushusha joto kama vile paracetamol (Panadol), si hatua mbaya ya kuchukua ispokuwa tatizo ni pale joto la mwili linapopanda mara kwa mara kwa zaidi ya siku tatu mfululizo bila kuchukua hatua ya kumpeleka mtoto kituo chochote cha afya kilichopo karibu.

Tuangalie nini maana ya jotomwili (body temperature).

Jotomwili  ni kipimo cha uwezo wa mwili kutengeneza joto, ambapo mwili hutengeneza joto kulingana na msawazo unaotakikana hata kama joto la nje ya mwili yaani mazingira yanayotuzunguka yatabadilika.

Inakuaje ya mwili unachemka?

Joto la mwili linapopanda kuliko kawaida ni kwamba mishipa ya damu (blood vessels) katika ngozi hutanuka na kubeba joto jingi kwenye ngozi ya mwili na kuanza kutokwa jasho kupita kiasi. Na tunaposema homa tunamaanisha kupanda kwa jotomwili (fever).

Ipi njia sahihi ya kutambua jotomwili limepanda?

Kuna njia ya asili ambayo tumeshaizoea kuitumia kugundua jotomwili limepanda au la, kwa kutumia sehemu ya juu ya kijanja cha mkono (dorsum) na kugusicha kwenye mwili wa mgonjwa. Ni njia nzuri ya awali katika kugundua jotomwili ispokuwa inakuwa ngumu kugundua joto la mwili limepanda kwa kiasi gani.

Njia iliyo ya uhakika ni kutumia kifaa kinachoitwa kipima joto (clinical thermometer), hiki ni kifaa kinachotumiwa hasa na wataalamu wa afya kwenye vituo vya afya. Kifaa hiki ni muhimu kwa kila familia kuwa nacho kwani ni rahisi kukitumia na kukielewa.

Utajuaje jotomwili limepanda kwa kutumia kifaa hicho (clinical thermometer)?

Kuna aina kama mbili za kipimajoto, ya kwanza ni mercury thermometer nay a pili ni digital thermometer. Kwa matumizi ya nyumbani ni vyema kutumia digital thermometer kwa urahisi wa kupata matokeo ya jotomwili.

Kiwango cha jotomwili.

Jotomwili la kwaida ni nyuzi joto 36.5 hadi 37.5, ikitokea kipima joto kikaonesha ni zaidi ya nyuzi joto 37.5 ni dalili ya kupanda kwa jotomwili, hivyo yakupasa kumpeleka mtoto kwenye kituo chochote cha afya kilichopo karibu.

Muhimu; 

Kupanda kwa jotomwili kwa watoto ni dalili ya hatari ukilinganisha na watu wazima, endapo hatua stahiki hazitachukuliwa hupelekea mtoto kupata degedege (convulsion), hivyo basi yakupasa kumpeleka kwenye kituo chochote cha afya kilichopo karibu yako.

Tukutane tena kwenye kipindi kijacho cha makala zinazohusu AFYA YA MTOTO siku kama ya leo, vilevile tutakutana kesho kwenye kipindi cha makala zinazoendelea.

Tunakutakia kila la kheri

Kwa maoni, ushauri, TIBA NA DAWA, Piga simu namba: 0652028582 au 0652394698 au 0654502550.

Whatsap group: Afya Ni Yangu,


Facebook Page: Afya Ni Yangu.


#TRIPLE MINDED.


 

Jaza form hii kupokea makala za Afya Ni Yangu.

* indicates required
Email Format