HUDUMA YA KWANZA (FIRST AID): Huduma ya kwanza ni nini?



Habari yako rafiki,

Leo ni siku nyingine tena tunakutana, leo ni jumamosi tulivu kabisa. Ni matumaini yetu kuwa unaendelea vizuri na unaendelea kuwa makini sana na afya yako kwa ujumla, na tunauhakika kuwa haupo tayari kuruhusu mtu/kitu chochote kicheze na afya yako. Ndiyo, afya yako ni ya thamani sana.

Leo tunaungana moja kwa moja kwenye kipindi chetu cha leo cha huduma ya kwanza (First Aid).

Huduma ya kwanza sio neno jipya kabisa katika masikio au macho yetu, tumeshalisikia sana na tumeshalizoea. Pia kuna baadhi yetu wamesha wahi kutoa huduma ya kwanza kwa mtu ambaye anahitaji kupatiwa huduma ya kwanza.
Ni vizuri sana kuwa na ujuzi wa kutoa huduma ya kwanza kwa kila mmoja wetu pale tu inapohitajika, leo tutachambua kwa kina kuhusu huduma ya kwanza.

Kwani huduma ya kwanzinakuaje/inafanyikaje?

Huduma ya kwanza ni msaada wa haraka sana unaotolewa kwa mtu yoyote ambaye yupo katika hali ya kuhatarisha au kupoteza maisha yake.

Huduma ya kwanza inaweza kutolewa kwenye dharula kama zifuatazo; mtu alikunywa sumu, aliyeng’watwa na nyoka (Nge, Nyuki, au mdudu yoyote mwenye sumu kali), aliye ungua, aliyepatwa na jeraha lenye kutoa damu nyingi, aliyepatwa na kifafa, aliyepoteza fahamu ghafla, aliyezimia, aliye paliwa, aliye zama maji na dharula nyengine nyingi.

Ni kitu gani napaswa kuzingatia napotoa huduma ya kwanza?

Kwanza kabisa ni muhimu sana kujua mambo ya msingi kabla ya kutoa huduma ya kwanza.

1.   Hakikisha unaujuzi wa kutoa huduma ya kwanza kulingana na tukio husika, usijaribu kutoa huduma ya kwanza endapo huna ujuzi huo kwani yaweza kuongea hatari zaidi kwa mgonjwa na hata kwako pia.

2.   Hakikisha unapotoa huduma ya kwanza wewe unakuwa salama, kwani unaweza kutoa huduma ya kwanza ikapelekea kuhatarisha maisha yako pia.

3.   Hakikisha unakuwa na vifaa vinavyotumika kutolea aina husika ya huduma ya kwanza (kama inahitajiaka).

4.   Inapotokea dharula inayohitaji huduma ya kwanza, fanya yafuatayo;

a)   Yakupasa uchunguze au uulize nini kimetokea. Itakusaidia kujua uanzie wapi kulingana na dharula husika.
b)   Je, mazingira yanakuruhusu kutoa huduma ya kwanza?
c)   Mgonjwa yupo eneo salama ambalo linakuwezesha kutoa huduma ya kwanza pale alipo pasipo mgonjwa hudhurika zaidi?

Ikiwa kuna dharula imetokea na imeathiri zaidi ya mmoja yakupasa kuweka kipaumbele (Priorities) kulinana na hali zao.

Nitawezaje kuweka kipaumbele(priorities) endapo kuna watu wengi walipatwa na dharula na kila aliyedhurika anahitaji msaada?

Tukutane tena kwenye kipindi kijacho rafiki, tutaendelea na somo letu la huduma ya kwanza.
Tukutakie kila la kheri, tukutane tena kesho kwenye vipindi vya makala zinazoendea.

 Tunakaribisha maswali kuhusiana na somo letu la leo kuanzia sasa.
Karibu.

Kwa maoni, ushauri, TIBA NA DAWA, Piga simu namba: 0652028582 au 0654394698 au 0654502550.

Whatsap group: AFYA YA UZAZI NA MTOTO,
Facebook Page: AFYA YA UZAZI NA MTOTO.

#TRIPLE MINDED.


Jaza form hii kupokea makala za Afya Ni Yangu.

* indicates required

AFYA YA MTOTO (1); Homa kwa watoto


 

Habari rafiki,

Tunakubaliana kwa pamoja kuwa watoto ni sehemu ya furaha katika maisha ya ndoa, na hilo tunalisadiki kwa pamoja.

Linapokuja suala la maradhi hasa kwa watoto katika familia hupoteza furaha yote katika familia.

Leo tutakushirikisha kuhusu homa hasa kwa watoto. Homa sio ugonjwa, homa ni dalili ya ugonjwa.

Kumekuwa na baadhi ya wazazi wakiona watoto wao joto la mwili limepanda hutumia dawa za kushusha joto kama vile paracetamol (Panadol), si hatua mbaya ya kuchukua ispokuwa tatizo ni pale joto la mwili linapopanda mara kwa mara kwa zaidi ya siku tatu mfululizo bila kuchukua hatua ya kumpeleka mtoto kituo chochote cha afya kilichopo karibu.

Tuangalie nini maana ya jotomwili (body temperature).

Jotomwili  ni kipimo cha uwezo wa mwili kutengeneza joto, ambapo mwili hutengeneza joto kulingana na msawazo unaotakikana hata kama joto la nje ya mwili yaani mazingira yanayotuzunguka yatabadilika.

Inakuaje ya mwili unachemka?

Joto la mwili linapopanda kuliko kawaida ni kwamba mishipa ya damu (blood vessels) katika ngozi hutanuka na kubeba joto jingi kwenye ngozi ya mwili na kuanza kutokwa jasho kupita kiasi. Na tunaposema homa tunamaanisha kupanda kwa jotomwili (fever).

Ipi njia sahihi ya kutambua jotomwili limepanda?

Kuna njia ya asili ambayo tumeshaizoea kuitumia kugundua jotomwili limepanda au la, kwa kutumia sehemu ya juu ya kijanja cha mkono (dorsum) na kugusicha kwenye mwili wa mgonjwa. Ni njia nzuri ya awali katika kugundua jotomwili ispokuwa inakuwa ngumu kugundua joto la mwili limepanda kwa kiasi gani.

Njia iliyo ya uhakika ni kutumia kifaa kinachoitwa kipima joto (clinical thermometer), hiki ni kifaa kinachotumiwa hasa na wataalamu wa afya kwenye vituo vya afya. Kifaa hiki ni muhimu kwa kila familia kuwa nacho kwani ni rahisi kukitumia na kukielewa.

Utajuaje jotomwili limepanda kwa kutumia kifaa hicho (clinical thermometer)?

Kuna aina kama mbili za kipimajoto, ya kwanza ni mercury thermometer nay a pili ni digital thermometer. Kwa matumizi ya nyumbani ni vyema kutumia digital thermometer kwa urahisi wa kupata matokeo ya jotomwili.

Kiwango cha jotomwili.

Jotomwili la kwaida ni nyuzi joto 36.5 hadi 37.5, ikitokea kipima joto kikaonesha ni zaidi ya nyuzi joto 37.5 ni dalili ya kupanda kwa jotomwili, hivyo yakupasa kumpeleka mtoto kwenye kituo chochote cha afya kilichopo karibu.

Muhimu; 

Kupanda kwa jotomwili kwa watoto ni dalili ya hatari ukilinganisha na watu wazima, endapo hatua stahiki hazitachukuliwa hupelekea mtoto kupata degedege (convulsion), hivyo basi yakupasa kumpeleka kwenye kituo chochote cha afya kilichopo karibu yako.

Tukutane tena kwenye kipindi kijacho cha makala zinazohusu AFYA YA MTOTO siku kama ya leo, vilevile tutakutana kesho kwenye kipindi cha makala zinazoendelea.

Tunakutakia kila la kheri

Kwa maoni, ushauri, TIBA NA DAWA, Piga simu namba: 0652028582 au 0652394698 au 0654502550.

Whatsap group: Afya Ni Yangu,


Facebook Page: Afya Ni Yangu.


#TRIPLE MINDED.


 

Jaza form hii kupokea makala za Afya Ni Yangu.

* indicates required
Email Format

MFULULIZO WA MAKALA; VIPINDI VYA MAKALA VITAKAVYORUSHWA KILA SIKU YA WIKI KUPITIA MTANDAO WA ‘AFYA NI YANGU’.



1.  SWALI LA LEO
2.  AFYA BORA
3.  AFYA YA UZAZI
4.  AFYA YA MTOTO
5.  ONGEA NA MSHAURI
6.  MASWALI NA MAJIBU
7.  CHANGAMOTO YA SIKU
8.  KLIINIKI YA MAMA NA MTOTO
9.  HUDUMA YA KWANZA (FIRST AID)
10.              MEDICAL & SURGICAL CONDITIONS

SWALI LA LEO;
Ni kipindi kitakacho fanyika siku ya jumatano, swali ambalo litawekwa mezani na wataalamu wa afya (uongozi wa mtandao wa AFYA NI YANGU). Swali ambalo litakuhitaji ufikiri wa kina ili kupata jibu sahihi, majibu yote  yatakayojibiwa na wanachama wa kundi hili yatafanyiwa kazi na uongozi.

AFYA BORA;
Ni makala itakayo rushwa siku ya jumanne, hii ni aina ya makala itakayo kuongezea maarifa kiundani zaidi kuhusu umuhimu wa kuwa na afya bora, namna gani unaweza kuwa na afya bora wakati wote na kuimarisha afya yako kwa ujumla.

AFYA YA UZAZI;
Ni aina ya makala itakayorushwa siku ya jumatatu, hapa utapata kujifunza magonjwa ya aina yote ya uzazi kwa mwanamke na mwanaume  pamoja na tiba/dawa sahihi.

AFYA YA MTOTO;
Ni makala itayorushwa siku ya alhamisi, itakayozungumzia hasa afya pamoja na magojwa ya watoto kuanzia akiwa kijusi (fetus) – kichanga (Neonate/Infancy) – hadi miaka kumi na moja (Children). Ni siku muhimu sana kwani utapata kuyafahamu mengi kuhusu watoto, kwani watoto ni sehemu ya furaha katika maisha ndoa na familia kwa ujumla.

ONGEA NA MSHAURI;
Huu ni wakati wa mwanachama wa mtandao huu kupata fursa ya kuongea na mshauri moja kwa moja kwa kupiga simu, kwa siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tano asubuhi hadi saa nne usiku.
Ushauri utakaotolewa ni wa magonjwa ya aina yoyote ya binadamu na kupatiwa ushauri na ufumbuzi wa tatizo husika.

N.B. Hairuhusiwi kutuma ujumbe (sms), hivyo ujumbe utakaotumwa hautafanyiwa kazi na uongozi husika.

MASWALI NA MAJIBU;
Hapa mwanachama atapata fursa ya kuuliza maswali husiana na magonjwa ya aina yote ya binadamu, kipindi hiki ni kwa siku ya Ijumaa tu. Hapa mwanachama atapata fursa ya kuwasilisha swali lake kwa njia ya ujumbe wa wa maandishi (whatsap group, inbox) au kwa kupitia e mail yetu (afyaniyangu@gmail.com)..

CHANGAMOTO YA SIKU;
Hapa utapokea makala itakayo elezea suluhisho la miongoni mwa  changamoto  zinazowasumbuwa watu wengi kuhusu afya zao hasa wale wanaotufikia moja kwa moja na wale wanaotupigia simu pia. Makala hii itaandaliwa siku ya ijumaa pekee. Hivyo tutakushirikisha na tutajifunza kwa pamoja.

KLINIKI YA MAMA NA MTOTO;
Hii ni huduma maalamu itakayotolewa kwa mfumo wa makala kuelezea huduma anazopaswa kupewa mama mjamzito kuanzia anapoingia kliniki hadi anapotoka, vile vile huduma anazopewa mtoto pale anapoingia kliniki hadi kutoka.
Hapa utajifunza mambo mbalimbali kama vile;



  • ·         Maana ya kila huduma anayopewa mama mjamzito anapokuwa kliniki.

    ·         Maana ya kila hatua anayoifuata mama mjamzito anapokuwa kliniki.

    ·         Umuhimu wa dawa/chanjo anazopewa mama akiwa kliniki.

    ·         Elimu anayopewa maam akiwa kliniki.

    ·         Vipimo anavyotakiwa kufanyiwa anapokuwa kliniki na mengine mengi.

Huduma hii ya KLINIKI YA MAMA NA MTOTO itatolewa kwa njia ya mtandao wa facebook page na whatsap ‘Afya Ni Yangu’ kila jumapili kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nane mchana.

Itafanyikaje kupitia mtandao?

Hapa tutakuwa kliniki na mama, mwanamke na hata wananaume wenye kujali na kuthamini afya za wake zao au wanawake pamoja na mtoto wao mtarajiwa, ili kupata somo hili inakubidi mwanachama awe anatumia kifaa chochote kinachomuwezesha kuwa na mtandao wa kijamii kama vile smartphone au tablet ambapo anatakiwa kuwa online siku hiyo na wakati wa somo husika.

 Itakuwaje kama sipo online kwa muda huo?

Bado hujapoteza kitu moja kwa moja kwani endapo utafungua mtandao wako utakutana na somo lililokuwa likiendelea siku hiyo, ispokuwa utakosa fursa ya kuuliza swali kuhusiana na somo au kile kinachohusiana na Kliniki ya mama na mtoto badala yake sasa utaweza kuuliza swali hilo kwenye kipindi kijacho.

Je, huduma hiyo ni kwa ajili ya wanawake wajawazito na wenye watoto wadogo pekee?

Hapana, huduma hii ni muhimu sana kwa kila mtu yaani mwanaume na mwanamke kwani ni vyema kwa wakina baba kuelewa ni huduma gani ambazo wenzi wao hupewa pindi wanapokuwa kwenye chumba cha uchunguzi na huduma zote wanazopata wanapokuwa kliniki kwa ujumla.

HUDUMA YA KWANZA (FIRST AID)

Hiki ni kipindi ambacho utaweza kujifunza ni kwa namna gani unaweza kutoa huduma ya kwanza kwa mtu yoyote pale tu anapopatwa na tatizo la ghafla la kiafya linalohitaji huduma ya kwanza kabla ya kumfikisha kituo cha afya.
Hili somo ni muhimu sana kwani utakuwa unauwezo wa kuokoa maisha ya mtu endapo tatizo litatokea ghafla eneo lolote ulilopo kama vile nyumbani, shuleni, ofisini, mgahawani, shambani n.k
Maarifa haya utayapata siku ya jumamosi jioni, hivyo utapaswa kuwa makini na somo hili.

MEDICAL & SURGICAL CONDITIONS

Hapa sasa ni ule wakati wakujifunza magonjwa ya kitabibu (kisukari, nimonia, kifua kikuu, mafua, UTI, malaria n.k) na magonjwa ya upasuaji (Kidole tumbo, kuziba kwa utumbo wa chakula, uvimbe n.k
Utapokea maarifa kwa undani zaidi kuhusu magonjwa haya, ambapo itakusaidia kugundua ugonjwa husika, dalili, vipimo vinavyohusika kugundua ugonjwa, tiba yake, namna ya kuepukana na ugonjwa husika.

MUHIMU:

Huu ni utaratibu mpya kabisa wa mfululizo wa masomo ya afya, kwa hakika tutakushirikisha maarifa hayo muhimu sana katika maisha yako ya kila siku na baada ya muda utakuwa na uelewa mpana kuhusu afya na hautakuwa hapo ulipo sasa kifikra. Huu mfumo mpya wa makala za afya umeandaliwa baada ya kufanyia kazi changamoto nyingi tulizokuwa tukipokea, hivyo tunaimani kuwa changamoto ni nyingi ila tutahakikisha tunazifanyia kazi kadri ya uwezo wetu.

Shabaha yetu kubwa ni kuhakikisha unakuwa na AFYA BORA YENYE UHAKIKA siku zote na wakati wote.

TRIPLE MINDED.




Jaza form hii kupokea makala za Afya Ni Yangu.

* indicates required
Email Format