HUDUMA YA KWANZA (FIRST AID): Huduma ya kwanza ni nini?



Habari yako rafiki,

Leo ni siku nyingine tena tunakutana, leo ni jumamosi tulivu kabisa. Ni matumaini yetu kuwa unaendelea vizuri na unaendelea kuwa makini sana na afya yako kwa ujumla, na tunauhakika kuwa haupo tayari kuruhusu mtu/kitu chochote kicheze na afya yako. Ndiyo, afya yako ni ya thamani sana.

Leo tunaungana moja kwa moja kwenye kipindi chetu cha leo cha huduma ya kwanza (First Aid).

Huduma ya kwanza sio neno jipya kabisa katika masikio au macho yetu, tumeshalisikia sana na tumeshalizoea. Pia kuna baadhi yetu wamesha wahi kutoa huduma ya kwanza kwa mtu ambaye anahitaji kupatiwa huduma ya kwanza.
Ni vizuri sana kuwa na ujuzi wa kutoa huduma ya kwanza kwa kila mmoja wetu pale tu inapohitajika, leo tutachambua kwa kina kuhusu huduma ya kwanza.

Kwani huduma ya kwanzinakuaje/inafanyikaje?

Huduma ya kwanza ni msaada wa haraka sana unaotolewa kwa mtu yoyote ambaye yupo katika hali ya kuhatarisha au kupoteza maisha yake.

Huduma ya kwanza inaweza kutolewa kwenye dharula kama zifuatazo; mtu alikunywa sumu, aliyeng’watwa na nyoka (Nge, Nyuki, au mdudu yoyote mwenye sumu kali), aliye ungua, aliyepatwa na jeraha lenye kutoa damu nyingi, aliyepatwa na kifafa, aliyepoteza fahamu ghafla, aliyezimia, aliye paliwa, aliye zama maji na dharula nyengine nyingi.

Ni kitu gani napaswa kuzingatia napotoa huduma ya kwanza?

Kwanza kabisa ni muhimu sana kujua mambo ya msingi kabla ya kutoa huduma ya kwanza.

1.   Hakikisha unaujuzi wa kutoa huduma ya kwanza kulingana na tukio husika, usijaribu kutoa huduma ya kwanza endapo huna ujuzi huo kwani yaweza kuongea hatari zaidi kwa mgonjwa na hata kwako pia.

2.   Hakikisha unapotoa huduma ya kwanza wewe unakuwa salama, kwani unaweza kutoa huduma ya kwanza ikapelekea kuhatarisha maisha yako pia.

3.   Hakikisha unakuwa na vifaa vinavyotumika kutolea aina husika ya huduma ya kwanza (kama inahitajiaka).

4.   Inapotokea dharula inayohitaji huduma ya kwanza, fanya yafuatayo;

a)   Yakupasa uchunguze au uulize nini kimetokea. Itakusaidia kujua uanzie wapi kulingana na dharula husika.
b)   Je, mazingira yanakuruhusu kutoa huduma ya kwanza?
c)   Mgonjwa yupo eneo salama ambalo linakuwezesha kutoa huduma ya kwanza pale alipo pasipo mgonjwa hudhurika zaidi?

Ikiwa kuna dharula imetokea na imeathiri zaidi ya mmoja yakupasa kuweka kipaumbele (Priorities) kulinana na hali zao.

Nitawezaje kuweka kipaumbele(priorities) endapo kuna watu wengi walipatwa na dharula na kila aliyedhurika anahitaji msaada?

Tukutane tena kwenye kipindi kijacho rafiki, tutaendelea na somo letu la huduma ya kwanza.
Tukutakie kila la kheri, tukutane tena kesho kwenye vipindi vya makala zinazoendea.

 Tunakaribisha maswali kuhusiana na somo letu la leo kuanzia sasa.
Karibu.

Kwa maoni, ushauri, TIBA NA DAWA, Piga simu namba: 0652028582 au 0654394698 au 0654502550.

Whatsap group: AFYA YA UZAZI NA MTOTO,
Facebook Page: AFYA YA UZAZI NA MTOTO.

#TRIPLE MINDED.


Jaza form hii kupokea makala za Afya Ni Yangu.

* indicates required

No comments:

Post a Comment